Print

Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch.Dkt.Msafiri Joseph Mbilu amejumuika na Washarika wa Usharika wa Kana katika Ibada ya Jumapili ambapo Ibada hiyo pamoja na kuwa na matukio mbalimbali kumekuwa na Uzinduzi wa Harambee yenye lengo la kuchangisha jumla ya Sh 2,000,000,000 (Bilioni Mbili) ili kuimarisha Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU.

Katika Hotuba yake  aliyoitoa  kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela, Askofu Mteule Mch.Dkt. Mbilu alisema  imekuwa siku ya furaha kubwa  kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo alimkaribisha Mkuu huyo wa Mkoa katika Usharika wa Kana na Dayosisi kwa ujumla.

Askofu Mteule Mch.Dkt. Mbilu amesema kuwa katika kipindi cha takribani miaka 3 kumekuwa na changamoto kubwa ya Chuo kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU, kufungiwa udahili kutoka na matatizo mbalimbali ya kimfumo na yaki utendaji.Hata hivyo baada ya Uongozi mpya wa Dayosisi kuingia madarakani mwezi Novemba 2020 uongozi umejikita sana katika kuhakikisha  Chuo Kikuu cha SEKOMU kinasimama tena.

Pamoja na matatizo mbalimbali yanayo kikabili Chuo hiki Askofu Mteule Mch.Dkt. Mbilu amesema ni madeni makubwa katika mabenki,taasisi mbalimbali na watu binafsi wakiwepo watumishi.

Ili kuhakikisha Chuo hiki kinaondokana na changamoto iliyopo Dayosisi imeamua kuanzisha harambee kubwa (Major Fundraising) itakayo saidia kumaliza madeni ya Chuo Kikuu cha SEKOMU na hatimaye kuruhusiwa kurejea katika hali yake ya kawaida.Harambee hii ina lengo la kumfikia kila msharika mmoja mmoja ambapo yameandaliwa makadi mbalimbali ili washarika waweze kuchangia.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga amemshukuru Askofu mteule Mch. Dkt Mbilu na kusema Serikali kwa ujumla wanafarijika sana kwa namna Kanisa linavyohudumia  wa Tanzania Kiroho na kimwili huku akitolea mfano wa Hospital ya Bumbuli inayo milikiwa na KKKT-Dayasisi ya Kaskasini Mashariki inavyo toa huduma nzuri kwa jamii.

Mkuu wa mkoa wa Tanga ameahidi kushirikiana na Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ili kuona Chuo kikuu cha SEKOMU kinarudi katika hali yake ya kawaida huku akipongeza namna ya uongozi uliopo unavyo endelea kuhakikisha unafanyia kazi maelekezo yaliyo tolewa na Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU).

Mhe.Martin Shigela amesema kukosekana kwa Chuo Kikuu cha SEKOMU ni changamoto kwa Mkoa wa Tanga kwa ujumla, nakuahidi kuwashirikisha wadau mbalimbali wenye lengo la kuona Chuo Kikuu cha SEKOMU kinarudi katika hali yake.

Mhe Mkuu wa Mkoa wa Tanga ameahidi kutoa Sh 5,000,000 Milioni tano huku jumla ya ahadi zote zilizo patikana katika uzinduzi huo ni jumla ya Sh 13,975,000 milioni kumi na tatu lakitisa na sabini na tano elfu.

Kwa upande mwingine Bi.Judica H. Omari Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga amesema anatambua uhusiano mzuri kati ya Kanisa na  Serikali huku akisema Serikali imekubali kupeleka vifaa pamoja na wahudumu katika Hospitali zinazo milikiwa na Kanisa  huku akiahidi kuwa sasa wanaenda kufanya kazi kuhakikisha Chuo Kikuu cha SEKOMU kinarudi huku akionesha umuhimu wa Chuo Kikuu cha SEKOMU katika Mkoa wa Tanga.

 

Bi.Judica H. Omari Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga

 Wengine walioshiriki katika ibada hiyo ni Bi,Kissa Gwakissa Kasongwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mkuu wa Jimbo Mteule  wa Jimbo la Pwani Mch. Thadeus Ketto,Mchungaji mwenza wa Usharika wa Kana Mch. Anna Msisili na Bw. David Chanyeghea Kaimu Mkurugenzi wa Uchumi,Mipango  na Maendeleo KKKT-DKMS.

 

Bi,Kissa Gwakissa Kasongwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe

Mkuu wa Jimbo Mteule wa Jimbo la Pwani Mch Thadeus Ketto

 

Mchungaji mwenza wa Usharika wa Kana Mch. Anna Msisiri

.........................................................

 

Hits: 10374