Mkutano Mkuu maalumu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki unaendelea kwa siku ya pili leo Machi 12, 2021 kwenye ukumbi wa Benjamini Mkapa katika Chuo cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa SEKOMU.

Askofu mteule wa KKKT DKMS Mch.Dkt. Msafiri Mbilu (Aliye simama) akitoa taarifa fupi ya utendaji kazi baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo 26/11/2020 na kuanza utendaji 1/12/2020 takribani siku 100 sasa.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KKKT DKMs wakifuatilia kwa umakini mjadala kuhusu mchakato wa kubadili katiba

............................................................

Askofu Mstaafu Joseph Jali wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kutoka kulia, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Januari Lugangikwa.