Print

Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu pamoja na viongozi wengine wa Dayosisi watatembelea Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) tarehe 28/03/2021 ambapo watashiriki na kuongoza Ibada katika baadhi ya sharika za DMP.

Mara baada ya Ibada, uongozi wa KKKT-DKMs na wenyeji wao watapata nafasi ya kukutana na Washarika wazawa kutoka Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, pamoja na Washarika kutoka Sharika za KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani wanaosali katika sharika  za DMP, katika kikao kitakachofanyika  Usharika wa Mbezi Beach, Tarehe 28/03/2021 majira ya Saa nane mchana (08:00).

Pamoja na mambo mengine yatakayo jadiliwa katika kikao hicho, uongozi utapata nafasi ya kukutana na kubadilishana mawazo na kuelezea zaidi juu ya Harambee kubwa inayo endelea katika Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Hata hivyo uongozi unaendelee kuwakumbusha wana Dayosisi waliopo ndani na nje ya Dayosisi kuwa, kilele cha Harambee hii kubwa kwa awamu ya kwanza kitafanyika tarehe 25/04/2021 katika Usharika wa Korogwe jimbo la Tambarare.

Uongozi unashukuru kwa ushirikiano mzuri unao endelea kati ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na wote wanaoendelea kuratibu na kuombea siku hii.

Harambee hii pamoja na malengo mengine inakusudia kukusanya fedha zitakazo saidia  kukirejesha Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) .

Hits: 9297