Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch.Dkt.Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 10 Aprili, 2021 amekutana na wana Dayosisi  wazawa kutoka Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, marafiki na wadau mbalimbali  wanaoishi katika Mkoa wa Kilimanjaro na maeneo mengine ya jirani na kufanya kikao  katika ukumbi wa Umoja Hostel Mkoani humo ambapo amepata nafasi yakuelezea hali ya Dayosisi ilivyo, huku kukishuhudiwa muamko mkubwa kutoka kwa wana Dayosisi hao.Ambapo wamepata nafasi ya kuchangia na kushauri mambo mbalimbali yatakayo leta mafanikio katika Dayosisi.

Askofu Mteule Mch.Dkt.Mbilu amewashukuru kwa kuonesha moyo na nia thabiti ya kushirikiana na washarika pamoja na marafiki  wengine kutoka Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na wadau.
Ameongeza  kuwa lengo la kukutana ni kupata nafasi ya kuelezea juu ya hali ya Dayosisi na kuahidi uwazi katika uendeshaji wa Dayosisi na kuhakikisha ripoti za vyanzo  vyote vya mapato vinawafikia washarika kila baada ya miezi mitatu.



Kilele cha harambee hiyo kwa awamu ya kwanza kitafanyika tarehe 25 Aprili,2021 katika usharika wa Korogwe jimbo la Tambarare kwa  lengo la kukusanya Tsh. Bilioni mbili (2,000,000,000.)

Mch. Dkt. Msafiri Mbilu  ameambatana na Msaidizi wa Askofu Mteule Mch. Michael Kanju,Kaimu Katibu Mkuu Mch.Godfrey T. Walalaze pamoja na ndugu David Chanyenghea ambae ni Kaimu mkurugenzi wa Uchumi na Mipango.