Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu aliye ambatana na Msaidizi wa Askofu Mteule Mch. Michael M. Kanju,Kaimu Katibu Mkuu Mch.Godfrey T. Walalaze,ndugu David Chanyenghea ambae ni Kaimu mkurugenzi wa Uchumi na Mipango  wamepata nafasi ya kushiriki katika ibada  ya jumapili iliyofanyika katika Kanisa la  KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati Usharika wa Arusha mjini-Kanisa Kuu leo tarehe 11 Aprili, 2021 .

 


Askofu Mteule Mch.Dkt.Mbilu ndiye aliye hubiri  neno la Mungu katika ibada hiyo huku akisoma neno kutoka kitabu cha 1 Yoh. 4:1-6 lililo beba ujumbe Yesu Kristo Ajifunua Kwetu. KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati inaongozwa na Baba Askofu Dkt.Solomon Jacob Massangwa.

............................

Mch.Sinyati Laizer Mchungaji Kiongozi KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati Usharika wa Arusha Mjini-Kanisa Kuu