Print

Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch.Dkt.Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 11 Aprili, 2021 ameendelea kukutana na kufanya kikao na marafiki,wadau na wanadayosisi wanao ishi   katika Mkoa wa Arusha na maeneo ya jirani katika ukumbi wa mikutano wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati Usharika wa Engarenarok lengo likiwa ni  kuwapa taarifa juu ya hali ya Dayosisi ya Kaskazni Mashariki.

Awali Askofu Mteule wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amesali katika Kanisa la KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Kati Usharika wa Arusha mjini akiambatana na  viongozi wengine wa Dayosisi.

Msaidizi wa Askofu Mteule Mch. Michael Kanju kwa niaba ya uongozi katika itikio ameseme wamepokea ushauri mawazo na maoni nakwenda kuyafanyia kazi ili kuona kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele. Ameongeza kuwa Dayosisi imezaliwa upya na mambo sasa yataenda vizuri na kwauwazi mkubwa ameendelea kuomba ushirikiano kwani uongozi utasimamia mali za Dayosisi na kuweka mifumo imara itakayo linda mali za Dayosisi.

 

 

Hits: 9502