Mchungaji Frank Richard Mntangi ameingizwa kazini kuwa Mkuu wa Jimbo la Tambarare KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi kilichofanyika tarehe 26/11/2020 kilimchagua Mchungaji Frank Richard Mntangi kuwa Mkuu wa Jimbo kwa kufuata Kanuni ya VIII ya Katiba  ya KKKT DKMS.

Alitangazwa wazi na kupokelewa rasmi katika Mkutano Mkuu wa Dayosisi uliofanyika Kanisa Kuu Lushoto (Cathedral) tarehe 25-27/11/2020.

Mchungaji  Frank Richard Mntangi ameingizwa kazini na Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 06/06/2021 katika Usharika wa Korogwe.

Jimbo la Tambarare lina jumla ya Sharika 16, Usharika wa Korogwe, Usharika wa Emau, Usharika wa Ebenezer, Usharika wa Mombo, Usharika wa Kwalukonge, Usharika wa Edeni-Kilindi, Usharika wa Handeni, Usharika wa Mkata, Usharika wa Mshihwi, Usharika wa Hale, Usharika wa Muheza, Usharika wa Bethel, Usharika wa Amani, Usharika wa Sinai, Usharika wa Kabuku pamoja na Usharika wa Songe.