Mchungaji Thadeus A. Ketto ameingizwa kazini kuwa Mkuu wa Jimbo la PWANI KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ikumbukwe katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi kilichofanyika tarehe 26/11/2020 kilimchagua Mchungaji Thadeus A. Ketto kuwa Mkuu wa Jimbo kwa kufuata Kanuni ya VIII ya Katiba  ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Alitangazwa wazi na kupokelewa rasmi katika Mkutano Mkuu wa Dayosisi uliofanyika Kanisa Kuu Lushoto (Cathedral) tarehe 25-27/11/2020.

Mchungaji Thadeus A. Ketto ameingizwa kazini na Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 13/06/2021 katika Usharika wa Kana.

...............