Leo tarehe 20/06/2021 imekua siku ya kihistoria kwani Mungu ametupa neema kwa kubarikiwa  na kuwekwa wakfu watheologia wanne (4) kuwa Wachungaji.Ibada imefanyika katika Kanisa  Kuu Lushoto (Cathedral).

Waliobarikiwa na kuwekwa wakfu ni Mch.Gibson Agrey,Mch.Daniel Warisha, Mch. Timilai Shenkalwa pamoja na Mch. Habil Kipande.

 

Ibada iliongozwa na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na Liturgia iliongozwa na msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  Mch.Michael M. Kanju.

Akizungumza katika ibada hiyo, Baba Askofu Dkt. Mbilu aliwataka wachungaji hao waliobarikiwa kusimamia na kutoa mafundisho sahihi ya Neno la Mungu hasa katika nyakati hizi ngumu zilizo jaa mafundisho potofu ya Neno la Mungu,pamoja na hayo mmoja wa Wachungaji walio barikiwa Mch. Timilai Shenkalwa ndiye aliye hubiri neno la Mungu huku akikumbusha juu ya kufanya kazi ya Mungu kwa umoja na kumtanguliza  Mungu mbele katika mambo yote.