Print

Tarehe 26/06/2021 imekuwa siku ya furaha katika Dayosisi  yetu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,  ambapo katika Jimbo la Kusini tumekuwa na Ufunguzi wa Kanisa katika  Usharika wa Msongolo mtaa wa Sinai.Katika ufunguzi huo Ibada  iliongozwa na Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu .

Ibada ilihudhuriwa na, Wachungaji, Wainjilisti, Mashemasi, Kwaya mbalimbali, Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Msongolo Mtaa wa Sinai.

Usharika wa Msongolo una jumla ya mitaa saba ambayo ni Msongolo,Zeba,Sinai,Funta,Kwemilungu,Nazareth pamoja na Yeriko, Mtaa wa Sinai ulitokana na mtaa mama wa Msongolo, Kabla ya kuanzishwa mtaa huo Wakristo walikuwa wakiabudu kwenye mtaa wa Msongolo

Mwaka 1977 Wakristo waliongezeka na kufikia 25 ndipo walipoomba na kuanzisha mtaa huu na ukaitwa Mtindilo,Wakristo hao waliabudu kwenye chumba cha darasa katika Shule ya Msingi Tekwa.mnamo mwaka 1978 waliomba kupatiwa  kiwanja kwenye ofisi ya Kijiji cha Tekwa  na walifanikiawa kupata kiwanja hicho.Mwaka 1979 walianza ujenzi wa Kanisa dogo na kumaliza ujenzi huo mwaka 1985 na kuhamia kwenye eneo la sasa na  ndipo walipo badili jina la mtaa huu na kuitwa SINAI.Ushariku huu unaongozwa na Mch. Mary Charamila

Hits: 9681