Msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Michael Mlondakweli Kanju ametoa pongezi kwa wafanyakazi wa vituo vya Nyumba ya masista (Nkwenda Mother House), Chuo cha Maarifa ya nyumbani Nkwenda,Shule ya msingi Tumshubire pamoja na Chuo cha Biblia Nkwenda kwa kazi nzuri wanayoifanya katika uendeshaji na utunzaji wa vituo hivyo

Pongezi hizo amezitoa leo tarehe 28/06/2021 katika mwendelezo wa ziara yake katika Dayosisi ya Karagwe

Akiwa katika nyumba ya masista,msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Michael Mlondakweli Kanju pamoja na mwenyeji wake msaidizi wa Askofu KKKT Dayosisi ya Karagwe Mch Yared A. Wakami walipewa zawadi ya mashati ya kufanana kama ishara yakuwa mapacha katika utumishi wao,zawadi hizo ni alama ya ukumbusho kwa kufika katika nyumba hiyo.

Picha hii ya ndege iliyoandikwa Air Tumushubire inamaanisha  mtoto akifika sehemu hii basi ndoto zake za kufika mbali zinatimia na hii ni imani kuwa undugu kati ya Dayosisi hizi mbili utaendelea na kufika mbali zaidi.