Askofu Dkt.Msafiri Joseph Mbilu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki leo tarehe 01/07/2021 ameshiriki kwenye Ibada ya ufunguzi wa mkutano mkuu (SINODI) KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi-Bukoba Jimbo la Kaskazini (A) Kigarama.Baba Askofu Dkt Msafiri Mbilu hapo kesho anatarajiwa kutoa mada kutoka kitabu cha Luka 14:28.Baba Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu ndiye mnenaji mkuu katika mkutano huo.

Ibada ya ufunguzi imeongozwa na  Askofu Dkt. Abednego Keshomshahara, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi-Bukoba

Katika picha Askofu Dkt.Msafiri Joseph Mbilu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (Kushoto) akiwa na Askofu Dkt. Abednego Keshomshahara, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi-Bukoba.