Leo tarehe 04/07/2021 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa Usharika wa Ngwelo Jimbo la Kaskazini, ambapo vijana wapatao 30 walibarikiwa. Ibada hiyo iliongozwa na Mkuu wa Jimbo la Kaskazini Mch Anderson Kipande, na Msaidizi wa Baba Askofu, Mch Michael M. Kanju alihubiri neno la Mungu.

Ibada ilihudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti,Mashemasi, Kwaya,Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Ngwelo ,

 

Vijana waliopata kipaimara walitoa kiasi cha Tsh 90,000/= kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za KKKT-Dayosisi ya Kaskani Mashariki katika masuala ya elimu.Aidha wamewashukuru  watumishi wa usharika  kwa kuwatufundisha Neno la Mungu kwa usahihi, katekisimo ndogo ya Daktari Martin Luther, masomo mbalimbali yanayohusu imani  ya Kikristo,na shughuli za utunzaji wa mazingira. Shukrani zao pia wamezitoa kwa  wazazi kwa kuwalea katika imani  ya kikristo na kufanikisha siku kuu hii. 

On 04th of July 2021 it was an extremely blessed day for the congregants of Ngwelo Lutheran Parish in which 30 youths confirmed their faith during the Sunday worship service.

The superintendent of Northern District, Rev. Anderson Kipande led the liturgy and the assistant to the Bishop of the ELCT- North Eastern Diocese Rev. Michael Kanju preached the word of God.

The ceremony was attended by Pastors, Evangelists, Deacons, choirs, civil servants and Congregants within and outside the parish.

In their speech to the Bishop, the confirmands contributed Tsh 90,000/= as the support to the ELCT North Eastern Diocese for her efforts in improving educational services.