Kaimu katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  anasikitika kutangaza kifo cha Bi. Catherine Mlondakweli Kanju ambaye ni mama mzazi wa msaidizi wa Askofu Mch.Michael Mlondakweli Kanju,kilichotokea leo Alhamisi  tarehe 22/07/2021 katika  kituo cha afya cha  St Joseph  Kwamndolwa Korogwe Tanga alikokuwa anapatiwa matibabu.Mazishi yatafanyika siku ya Jumatatu tarehe 26/07/2021 Saa sita mchana nyumbani kwao Lutindi.Uongozi unatoa pole kwa Baba Dean Mch. Michael Mlondakweli Kanju, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.