Kaimu katibu Mkuu wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa niaba ya uongozi wa KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki  anasikitika kutangaza kifo cha mke wa marehemu Mch. Yohana  Nyaki, Mama Makinyemi Y. Nyaki kilichotokea leo tarehe 30/07/2021 nyumbani kwao Fuizai, mazishi yatafanyika siku ya kesho mchana  tarehe 31/07/2021 na Ibada ya mazishi itafanyika  katika Usharika wa Fuizai .

Uongozi unatoa pole kwa familia ya marehemu Mch.Yohana  Nyaki, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.