Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu leo tarehe 08/08/2021 ameongoza Ibada ya Jumapili katika Usharika wa Mombo mtaa wa Buiko.

Askofu Dkt. Mbilu alipata wasaa wa kufungua nyumba ya mtumishi ambayo ujenzi wake ulianza mwaka 2017 baada ya kuona uhitaji mkubwa wa kuwepo nyumba kwaajili ya mtumishi ili kupunguza gharama za kukodisha nyumba.

 

WASHARIKA WA USHARIKI WA MOMBO MTAA WA BUIKO

Awali alifanyika Ibada ya ufunguzi wa Kanisa katika Usharika wa Mombo Kanda ya Buiko- Mtaa wa Manga Mikocheni. Kanisa lililo asisiwa mwanzoni mwa mwaka 2005 na hii ni baada ya washarika wa Manga mikocheni kujiunga kutoka Buiko mahali walipokuwa wanaabudu na ujenzi bado unaendelea

WASHARIKAWA WA USHARIKA WA MOMBO KANDA YA BUIKO- MTAA WA MANGA MIKOCHENI