Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch.Dkt.Msafiri Joseph Mbilu amekutana na kufanya mazungumzo na Mch.Dkt.Ulrich Mouller (Vice moderator UEM) ambaye aliambatana na Mch.Dkt. Ernest Kadiva (The deputy Executive secretary in Africa) Leo tarehe 14/08/2021 alipo tembelea makao makuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

 

Mch.Dkt.Ulrich Mouller akiwa katika kiwanda cha uchapishaji  cha Vuga Press Publishing House, ambapo amejionea namna kiwanda hiki kinavyo fanya kazi na kupokea maelezo ya kina juu ya mipango inayoendelea  kukirudisha kiwanda hiki  katika hali yake ya awali.

 

 ........

Mch.Dkt.Ulrich Mouller (wa pili kutoka kulia) akipokea maelekezo kutoka kwa Dkt. Yekenya (Wa kwanza kutoka kulia) punde alipo tembelea Hospitali ya Bumbuli inayo milikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

 

UEM: United Evangelical Mission ni chama Cha kiinjili Cha kimisioni kilichoanzishwa miaka 25 iliyopita na wamisionari kutoka Ijerumani wa Rhenish na Betheli ambao walifika Africa, na Asia kwa ajili ya kuanzisha shughuli za Dini. Katika Africa walifika katika Nchi 7 amabazo ni Tanzania, DR Congo, Africa ya Kusini, Botswana, Cameroon na Namibia na Rwanda kukiwa na madhehemu 15.Katika Tanzania inawakilishwa na Makanisa 4 ya KKKT ambayo ni KKKT Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na KKKT Dayosisi ya Karagwe.

 ..............