Leo tarehe 12/09/2021 imekuwa siku ya baraka kwa washarika wa Usharika wa Kisosora Jimbo la Pwani. Ambapo imefanyika Ibada iliyokuwa na matukio mbalimbali vijana wapatao 19 wamepata kipaimara na wawili kati yao walibatizwa.

Liturgia katika Ibada hiyo iliongozwa na Mkuu wa jimbo la Pwani Mch. Thadeus A. Ketto, na Baba Askofu Dkt.Msafiri Joseph Mbilu alihubiri neno la Mungu.

Ibada ilihudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti, Mashemasi, Kwaya, Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya usharika wa Kisosora.

Picha rasmi ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki itakayo tumika katika Ofisi za KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.