Print

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani Mch Dkt. Alex Malasusa amewakumbusha waimbaji kuwa uimbaji unamchango mkukwa katika kumuita mtu kwa mungu na uimbaji umetumika kama chombo cha uinjilisti hivyo kukuwa kwa injili katika KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na sehemu nyingine upo mchango mkubwa wa waimbaji.

Askofu Dkt.Malasusa ameyasema hayo leo tarehe 24/10/2021 na kuongeza kuwa waimbaji wasisahau kuwa wanahitajika kuishi maisha yanayo mpendeza Mungu ili waweze kwenda kuishi maisha ambayo Yesu amekwenda kuwaandalia huku akishukuru kwa ushirikiano mzuri uliopo kati ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki pamoja na KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani,

 

Katika Ibada hiyo Askofu Dkt. Alex Malasusa ndiye aliyekuwa mgeni rasmi na alihubiri neno la Mungu.

 Katika Ibada hiyo kubwa ya maadhimisho ya miaka 60 ya Kwaya Kuu ya  Kanisa Kuu Lushoto tangu kuanzishwa kwake, katika kuweka alama ya Jubelee hiyo Kwaya Kuu wamenunua Coaster ambayo itafanya kazi ya Uinjilisti.

Hits: 9105