Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea;Nitakushauri,jicho langu likikutazama.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt.Msafiri Joseph Mbilu amewataka viongozi walio pewa dhamana ya kusimamia mali za Dayosisi  kuendelea kuwa mawakili wema kwa kufanya kazi kwa uamainifu, uadilifu na uwazi kwakuwa wameaminiwa na yeyeto atakayefanya tofauti  lazima ataulizwa.

Askofu Dtk Msafiri Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 14/11/2021 kwenye Ibada ya Kipaimara iliyofanyika katika Usharika wa Vuga Jimbo la Kusini na kusema kuwa ni lazima kufanya kazi kwa uwazi na kwa bidii ikiwemo matumizi sahihi ya fedha za Dayosisi ili kuleta mabadiliko chanya katika utumishi wao na Dayosisi kwa ujumla.

Katika Risala yao iliyosomwa mbele ya Baba Askofu Dkt. Mbilu vijana hao wa kipaimara wamesema wameona juhudi mbalimbali zinazofanywa na uongozi wa Doyosisi katika kuirejesha Dayosisi katika hali nzuri, na hivyo vijana hao kuungana na Baba Askofu katika juhudi hizo kwakutoa jumla ya Tsh.375,000. Jumla ya vijana 97 wamebarikiwa.

 

Katika hatua nyingine Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu, mara baada  ya Ibada, ametembelea Seminara ndogo ya Bangala inayo milikiwa na K.K.K.T- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na kufanya maombi maalumu kwaajili ya wanafunzi ambao wanatazamia kufanya mitihani ya kuhitimu kidato cha nne  tarehe 15.11.2021 Nchi nzima huku akiwataka kumtanguliza Mungu katika  mitihani hiyo.