Print

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewashukuru Washarika wa Usharika wa Kange Mtaa wa Maweni kwa namna wanavyo jitoa katika kazi za umoja.

Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo leo tarehe 27/08/2022 kwenye Ibada ya Shukrani  iliyotanguliwa na uwekwaji wa jiwe la msingi la Darasa la Watoto wa Shule ya Jumapili (Sunday School) , katika Mtaa wa Maweni Usharika wa Kange.

Askofu Dkt. Mbilu amesema ni jambo la baraka kwa Sharika na mitaa ya Jimbo la Pwani kuendelea kuwa na moyo wa kujitoa katika kazi za umoja ikiwemo uchangiaji wa deni linalo ikabili Dayosisi.

Hata hivyo Askofu Dkt. Mbilu amewasihi Wachungaji kuendelea kuwahimiza Washarika kukamilisha viwango vyao walivyo ahidi   kabla ya awamu ya kwanza ya uchangiaji itakayo kamilika tarehe 31/10/2022 kulingana na barua ya Baba Askofu kwa Washarika na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Hits: 6233