Print

"Pandeni milimani, Mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana".Hagai 1:8. Leo tarehe 03/09/2022 Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu  ameongoza   harambee ya ujenzi wa Kanisa katika Usharika wa Kabuku, Jimbo la Tambarare. Askofu Dkt. Msafiri Mbilu alianza harambee hiyo kwa   kutoa kiasi cha  Tsh. 200,000/= (LAKI MBILU). Baada ya harambee yote kufanyika kiasi cha Tshs. 17,695,000/= kilipatikana  Ikiwa ni fedha taslimu  Tshs. 14,695,000/ huku ahadi ikiwa  Tshs. 3,000,000/=

Hits: 5900