Print

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewashukuru Washarika wa Usharika wa Shume kwa mambo mengi na mazuri wanayoyafanya ya kuijenda Dayosisi na kipekee mchango mkubwa ambao wanaendelea kuutoa kwaajili ya uchangiaji wa Deni la Dayosisi.

Askofu Dkt. Mbilu ametoa shukrani hizo leo tarehe 04/09/2022 akiwa kwenye Ibada ya Jumapili iliyokuwa na tendo la kuwabariki vijana wa kipaimara, akiwa katika Usharika huo ambao ndio unaoongoza katika uchangiaji wa Deni la Dayosisi katika Jimbo la Kaskazini amewasihi  kuendelea na juhudi hizo ili kufikia mwisho wa uchangiaji   wa Deni hilo kwa awamu hii ya kwanza wawe wamemaliza kiasi walichopangiwa.

“Na mimi nawashukuru sana kwakua mmeendelea kuchangia na mtaendela kuchangia kwaajili ya maendeleo ya Dayosisi yetu naomba tusirudi nyuma tuendelee kuchangia Deni hili” Aliongeza Askofu Dkt. Mbilu.

Katika Ibada hiyo  vijana wapatao 107 walibarikiwa mara baada ya kukamilisha safari yao ya mafundisho katika kipindi cha miaka miwili wamempongeza Baba Askofu Dkt. Msafiri Mbilu pamoja na Uongozi mzima kwa kuonesha jitihada za kulipa Deni la Dayosisi.

Wameongeza kuwa deni hilo limekuwa aibu katika jamii na Kanisa aidha wamemshukuru kwa jitihada zilizo saidia upatikana wa Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI)  kwani wanaamini Chuo hicho kitaleta uhai kwa manufaa makubwa hususani kwa vijana na jamii yote ya Watanzania na Afrika kwa Ujumla.

Chuo hicho chenye usajili wa NACTE kwa Namba. KOTETI/HAS/249 kwa sasa kinaenelea kupokea wanafunzi na wale wanao hitaji kujiunga na kozi ya ORDINARY DIPLOMA IN PHARMACEUTICAL SCIENCES (NTA LEVEL 6) – KWA MIAKA 3 wanaendelea kukaribishwa kutuma maombi yao. Sifa za kujiunga ni angalau alama D nne (4) ikiwemo masoma ya Biology na Chemistry na masomo mengine yoyote mawili (isipokuwa masomo ya Dini).

Vijana hao waliobarikiwa wamekiri kufundishwa mafundisho sahihi ya Neno la Mungu na kuahidi kutoyumbishwa na mafundisho ya uongo ya Neno la Mungu kwani wamepokea silaha kubwa ya Neno la Mungu ambayo itawasaidia kupambana na mwovu shetani.

Hits: 6554