Print

Leo tarehe 18/09/2022 Imekuwa siku ya baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Malibwi Jimbo la Kaskazini ambapo vijana wa Kipaimara wapatao 106 walibarikiwa na wa 3 kati yao walibatizwa, Ibada iliongozwa na Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Michael Mlondakweli Kanju katika

 Ibada iliyohudhuriwa na Wachungaji, Wainjilisti, Kwaya, Washarika pamoja na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Usharika wa Malibwi.

MKUU WA JIMBO LA KASKAZINI MCH: ANDERSON KIPANDE.

Awali kabla ya Ibada hiyo Msaidizi wa Askofu Mch. Michael  Kanju alizindua mnara wa Kengere na nyumba ya mtumishi katika Usharika huo wa Malibwi Mtaa wa Kwedeghe.

Msaidizi wa Askofu Mch. Michaele Kanju katika matukio hayo, amemuwakilisha Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ambaye yupo Nchini Ujerumani kwa ziara ya kikazi.

Aidha kufuatia kuitwa mbinguni  kwa Baba Mzazi wa Shemasi Rehema Mbura Mzee Solomoni Baraza  Msaidizi wa Askofu Mch. Michael Kanju amefika na kutoa pole kwa familia ya Marehemu Mzee Solomoni Baraza  .

Marehemu Mzee Solomoni Baraza aliitwa mbinguni tarehe 15/09/2022 na mwili wake utapumzishwa katika makaburi yaliyopo katika Mtaa wa Mshangai Mission Jumanne ya  tarehe 20/09/2022.

Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.

Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, unatoa pole katika kipindi hiki kigumu kwa familia  ya Marehemu Mzee Solomoni Baraza, ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na lihimidiwe.

 

Hits: 6554