Print

\

Sehemu ya Wajumbe wengine wa Kamati ya Uhusiano

PICHA YA PAMOJA mara baada ya mazungumzo ya Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu na Mkuu wa Jimbo la Vlotho Mch. Dorothea Goudefroy (wa pili kutoka kushoto) pamoja na wajumbe  wa kamati ya Undugu toka Vlotho.

Hili ni Kanisa la Dithmaschen lilojengwa mwaka 1200 . 

Siku ya Jumanne ya tarehe 20/09/2022 Baba Askofu pamoja na wenyeji wake  walitembelea Usharika wa Dithmaschen ulioko Kaskazini mwa Ujerumani kwenye bahari ya Kaskazini. Usharika huu una urafiki na Usharika wa Ngwelo ya Mlalo pia walisaidia fedha zilizowezesha  ujenzi wa bwalo la chakula katika  Shule ya Sekondari Lwandai inayomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

KATIKA PICHA Baba Askofu akiwa na Mama Lotte Boigs mara baada ya kukaribishwa nyumbani kwa mama huyu. Hata hivyo Mama huyu ni kiungo kikubwa cha urafiki huu.

KATIKA PICHA: Baba Askofu akiwa na Mama Lotte (Wa kwanza kushoto) pamoja  na Mwalimu Andrea (wa kwanza kulia) hawa wote ni wajumbe muhimu wa kamati ya Uhusiano.

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Hannover, Bishop Dr. Adelheid Ruck-Schöder.(wa pili kutoka kushoto)

KATIKA PICHA mara baada ya Jumapili ya tarehe 18/09/2022 iliyofanyika katika Usharika wa St. Jacobi Göttingen wenye uhusiano na Usharika wa Mlalo. Baba Askofu Dkt. Mbilu ndiye aliyongoza Ibada hiyo.Baada ya Ibada Baba Askofu  alipata nafasi ya kufanya mazungumzo na vikundi vya Urafiki,wakiwemo Mchungaji wa sharika, Wazee wa Kanisa na Viongozi wa Uhusiano.

Hits: 5736