Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch. Godfrey Tahona Walalaze leo Jumamosi ya tarehe 24/09/2022 ameongoza Ibada ya Kipaimara iliyofanyika katika Usharika wa Hengiti Mtaa wa Fuizai
ambapo jumla ya vijana wapatao 108 wamepata kipaimara huku wakikiri kufundishwa na kuifahamu misingi ya imani yao na kuahidi kuto yumbishwa na mafundisho ya uongo .
Awali Katibu Mkuu Mch. Walalaze akimuwakilisha Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu katika Ibada hiyo pia alizindua kwa upya mnara wa kengere ambao umefanyiwa marekebisho.