Print

MSAIDIZI WA ASKOFU KKKT-DKMs, MCH MICHAEL MLONDAKWELI KANJU

Msaidizi wa Askofu KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Michael Mlondakweli Kanju ametoa wito kwa wazazi na walezi kutuma watoto wao kujiunga na Chuo cha Kolowa Technical Training Institute kinachotoa Kozi ya Ufamasia (Pharmacy).

amesema kuwa ni vema kutumia muda wa udahili ulioongezwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kutuma maombi yao ilikujiunga na Chuo hicho.

Msaidizi wa Askofu Mch. Kanju ametoa wito huo leo tarehe 25/09/2022 kwenye Ibada ya Kipaimara iliyofanyika katika Usharika wa Malindi ambapo jumla ya vijana wapatao 108 walibarikiwa huku wawili kati yao wakibatizo.

Katika risala ya vijana hao waliobarikiwa wametoa shukrani zao za dhati kwa Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu na wasaidizi wake kwa kuona umuhimu wa elimu kwa kurudisha tena huduma ya kielemu katika Chuo cha KOTETI.

Chuo cha Kolowa Technical Training Institute kipo  Wilayani Lushoto Mkoani Tanga na kinamilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, huku kikiwa na usajili wa NACTE kwa Namba. KOTETI/HAS/249 na sasa kinatangaza nafasi ya masomo kwa muhula mpya wa SEPTEMBER-2022/2023 kwa siku mbilu yaani kuanznia tarehe 26-27 kwa kozi ya PHARMACY YAANI ORDINARY DIPLOMA IN PHARMACEUTICAL SCIENCES – KWA MIAKA 3.

Sifa za kujiunga ni angalau alama D nne (4) ikiwemo masoma ya Biology na Chemistry na masomo mengine yoyote mawili (isipokuwa masomo ya dini). Ada ni Tsh. 1,400,000/= na inalipwa kwa awamu. Hosteli na huduma za chakula zinapatikana kwa gharama nafuu.

Maombi yafanyike kupitia njia ya mtandao yaani ONLINE APPLICATION SYSTEM-Central Admission System (CAS), kwenye tovuti ya Chuo: www.koteti.ac.tz  au kupitia Tovuti ya NACTE:  www.nacte.go.tz

Hata hivyo muombaji anapaswa kuchagua Chuo cha Kolowa Technical Training Institute (KOTETI) kwenye orodha ya vyuo vitakavyo jitokeza kwenye mfumo. Kwa maelezo zaidi na maelekezo fika moja kwa moja kwenye Ofisi za Chuo zilizopo Magamba Lushoto Tanga Tanzania katika majengo ya kilipokuwa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastiani Kolowa (SEKOMU). CAMPUS “B”

Kwa mawasiliano zaidi ya simu: -      0712811420      au     0764105944       This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.  

Hits: 7100