Mch ,Emmanuel Mtoi ni mmoja wa wachungaji waliotumwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki kutumika katika iliyokuwa Mision ya Kigoma (KKKT-Dayosisi ya Magharibi Sasa). alifika katika Usharika wa Kasulu mwaka 2002 Julai na kutumika kwa miaka 10 katika Usharika huo. Aliteuliwa kuwa Mkuu wa Misioni mwaka 2007 nafasi aliyoitumikia kwa miaka 11. alitumika katika Usharika wa Kigoma kwa miaka 7 tangu mwaka 2012 hadi 2018 Aprili na hapo ndipo aliporejea nyumbani KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (TANGA). Mchakato wa kuanzishwa kwa Dayosisi ulianzia mikononi mwake Mch. Mtoi. Wachungaji 6 walisoma na kubarikiwa mikononi mwake. Mch Majoh naye akibarikiwa mikononi mwake hata hivyo upanuzi wa Kanisa Kuu la Dayosisi ya Magharibi sasa ni kazi yake aliyoifanya kwa ushirikiano mkubwa na Wakristo ndugu jamaa na marafiki . Ujenzi wa Ofisi za Dayosisi sasa, ujenzi wa madarasa 2, Ofisi ya kituo,jiko na vyoo vya kisasa ni miongoni mwa kazi alizozifanya Mch. Mtoi. Mungu akubariki Sana.