MKUU WA KKKT BABA ASKOFU DKT. FREDRICK ONAEL SHOO.
Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo leo tarehe 18/10/2022, amefungua mafunzo ya siku mbili yanayohusu utoaji wa huduma bora za Afya katika Hospitali na vituo vya Afya vinavyo milikiwa na KKKT.
Mafunzo haya yanafanyika Jijini Dodoma ambapo yamehudhuriwa na wajumbe kutoka Hospitali 23 na vituo vya Afya 24 vya KKKT. Wajumbe hao ni pamoja na maaskofu, makatibu wakuu pamoja na wataalamu wa Afya.
Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ni mmoja wa wajumbe wanaohudhuria katika mafunzo hayo.