KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA

DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI

S.L.P. 10 (SIMU 027 – 2660027 / FAX 027 -2660092) LUSHOTO

E-mail: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

UUZAJI WA MBAO ZA MIKARATUSI KATIKA SHAMBA LA KKKT -DKMs IRENTE-LUSHOTO

1) Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) itauza mbao aina ya Mikaratusi yenye jumla ya meta za ujazo 944.28 zilizopo katika shamba la Irente Wilaya ya Lushoto. Mbao hizo zitauzwa huko Irente mahali zilipo na hivyo wanunuzi wanaalikwa kufika huko.

2) Wanunuzi wanakaribishwa kutembelea shamba sehemu zilipo mbao tajwa wakati wa saa za kazi kuanzia saa tatu (3:00) asubuhi hadi saa tisa (9:00) alasiri siku za Jumatatu hadi Jumamosi. Meneja wa shamba husika au wasaidizi wake watakuwepo kwa ajili ya mauzo na pia kutoa maelezo ya ziada.3) Mnunuzi mwenye nia ya kununua mbao hizo baada ya kuainisha kiasi cha mbao anachotaka, na kukubaliwa kufanya malipo, ataonyesha risiti ya malipo yote toka Benki atakayoelekezwa na akaunti atakayopewa ili aweze kuchukua mbao zake.

4) Mnunuzi atatakiwa kuchukua mbao zake ndani ya siku 5 (tano) mara baada ya kufanya malipo.

5) Maombi ya tenda ya ununuzi wa mbao yaambatanishwe na risiri ya malipo ya Tsh: 50,000 Akaunti namba 41606600200 Jina la akaunti NED ELCT MAGARI NA MBAO na yatumwe kwa
Katibu Mkuu

KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki

S.L.P 10 LUSHOTO

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

6) Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12/11/2022 saa 10:00am.