Leo tarehe 12/11/2022 imekuwa siku ya furaha na baraka tele kwa Washarika wa Usharika wa Malindi Mtaa wa Kana Mpya ambapo Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ameongoza Ibada iliyokuwa na tendo la uwekwaji wa Jiwe la Msingi na ufunguzi wa Kanisa.KATIKA HISTORIA:- Ibada katika Mtaa huu wa Kana Mpya, zilianza rasmi mwaka 2012 nyumbani kwa mzee Shabani Vuri kwa miaka mitatu mnamo mwaka 2015 Usharika ulipata eneo ambalo ndipo lilipojengwa Kanisa lililo funguliwa leo.Kwa sehemu kubwa Mtaa huu wa Kana Mpya ulilelewa na Askofu Mstaafu Mzee Joseph Jali na ndipo alipomkabidhi Mch. Clement Tarimo kuendelea kuulea Mtaa huu, watumishi wengine walioendeleza kazi ya kulea Mtaa huu ni pamoja na Shemasi Shempuna, Mch. Daudi Mwangilagwa na sasa Mch. Walisha.Mtaa huu ulianza na Wakristo wasiozidi 5 na hadi sasa katika Mtaa huu kuna ongezeko la Wakristo 27 na kupelekea Mtaa kuwa na Wakristo 32 kati yao 20 ni Watoto wa Shule ya Jumapili.