KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mnamo tarehe 15/11/2022 ilipokea ugeni kutoka KKKT-Dayosisi ya Ulanga Kilombero kwa lengo la kujifunza na kudumisha undugu kati ya Dayosisi hizi mbili.

Msaidizi wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Ulanga Kilombero Mch. Paulson Samweli Matimbwi akisaini kitabu cha wageni .

Wameanza ziara yao leo tarehe16/11/2022 kwa kushiriki Ibada ya asubuhi pamoja na kutembelea Makao Makuu ya KKKT- Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Askofu.

Ziara hii itakua kwa muda wa siku 5, wakiongozwa na Mkuu wa Jimbo la Kusini Mch. Issai Mweta watapata wasaa wakutembelea Vituo pamoja na senta za Majimbo kwa kujifunza mambo mbalimbali yanayofanyika ndani ya Dayosisi yetu.

Msafara huu wa ugeni unaongozwa na Msaidizi wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Ulanga Kilombero Mch. Paulson Samweli Matimbwi ambaye ameambatana na Wakuu wa Majimbo , Mkuu wa Jimbo la Mlimba Mch. Essau Herode Wihagile,Mkuu wa Jimbo la Ulanga Mch. Wilson Samson Nyakachewa, Mkuu wa Jimbo la Ifakara Mch. Fadhili Gamalieli Mpolo pamoja na Mkuu wa Jimbo la Kilombero Mch. ELibariki Zabron Kisenime.