Leo tarehe 21/11/2022 Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mwl. Julius Samweli Madiga, ametambulishwa rasmi kwa wafanyakazi wa Ofisi Kuu ya KKKT-DKMs ambapo pia amepata nafasi ya kusaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Askofu. Atakua bega kwa bega na aliyekuwa Katibu Mkuu Mch. Godfrey Tahona Walalaze kwa muda wa mwezi mmoja kama moja ya taratibu ya kukabidhiana Ofisi.

KATIBU MKUU KKKT-DKMs,  MWL. JULIUS SAMWELI MADIGA.