Leo tarehe 15/01/2023 imekuwa siku ya   furaha na baraka tele kwa washarika wa Usharika wa Magamba ambapo, Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu  akiwa katika Jimbo la Kusini,ameongoza Ibada ya Jumapili iliyotanguliwa na  ufunguzi wa  Kanisa katika Usharika wa Magamba Mtaa wa Mabughai pamoja na uwekwaji wa jiwe la msingi katika madarasa ya Watoto wa Shule ya Jumapili (Sunday School) katika senta ya Usharika huo wa Magamba.