KUTOKA USHARIKA WA KANA TANGA: Leo tarehe 15/01/2023, Msaidizi wa Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch. Michael Mlondakweli Kanju ameongoza Ibada ya Jumapili  katika Jimbo la Pwani Usharika wa Kana.


Katika Ibada hiyo Mch. Emmanuel Mtoi alitambulishwa rasmi kuwa Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kana na kaimu Mkuu wa Jimbo la Pwani akichukuwa nafasi ya Mch. Thadeus Ketto ambaye sasa yupo Makao Makuu ya KKKT-DKMs kama Mratibu wa elimu na elimu ya Kikristo


Mara baada ya kupokea wajibu huo Mch. Mtoi amesema kuwa anamshukuru Mungu kwa nafasi hizo alizopewa ambazo kwake amezipokea kama deni na nikwa neema tu. Mch Mtoi alianza hudumu ya kumtumikia Mungu katika ngazi ya uinjilisti mwaka 1988 katika Usharika wa Kana.