KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA-DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI [KKKT-DKMs]z

 1. UTANGULIZI

Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni miongoni mwa Dayosisi 27 ndani ya KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-DKMs ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu. Taasisi hii inatoa tangazo la kazi kwa nafasi zifuatazo:

 1. AFISA MIPANGO WA DAYOSISI

MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI.

 1. Awe raia wa Tanzania.
 2. Awe na umri usiopunguza miaka 18 na usiozidi miaka 45.
 • Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato Cha Nne, Sita na Taaluma aliyosomea.
 1. Elimu kiwango cha kuanzia astashahada moja ya uchumi na fani zinazoendana na hizo kutoka vyuo vinavotambulika
 2. Awe na uzoefu usiopungua miaka mitatu
 3. Awe na uzoefu wa kubuni na kuandika miradi pamoja na usimamizi pmoja na tathmini.

MAOMBI YOTE YAAMBATANISHWE NA,

 1. Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
 2. Nakala ya cheti cha kidato cha nne au/ na cha sita au stashahada kulingana na kada ya mwombaji. Kwa aliyesoma nje ya nchi au mitaala ya nje ya nchi waambatanishe cheti cha ithibati kutoka baraza la mitihani Tanzania (NECTA).
 • Nakala ya vyeti vya Taaluma na Transcript, Aidha waliosoma vyuo vya nje ya nchi, waambatishe cheti cha Ithibati kutoka TCU.
 1. Wasifu (CV).
 2. Picha ndogo (passport size) moja ya hivi karibuni.
 3. Nakala ya kitambulisho cha uraia (NIDA/ Namba ya NIDA).
 • Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako Pamoja na cheti cha kuzaliwa na NIDA hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa viapo na kusajiliwa na Msajili wa hati, wizara ya Ardhi na maendeleo ya makazi.

 1. MRATIBU WA MADINI KKKT-DKMs

MASHARTI YA JUMLA YA WAOMBAJI WA KAZI.

 1. Awe raia wa Tanzania.
 2. Awe na umri usiopunguza miaka 18 na usiozidi miaka 45.
 • Awe na vyeti kamili vya mafunzo ya fani aliyosomea (Cheti cha Kidato Cha Nne, Sita na Taaluma aliyosomea.
 1. Elimu kiwango cha kuanzia astashahada na kuendelea ya miamba na madini Geology kutoka vyuo vinavyotambulika.
 2. Awe na nyaraka zote muhimu ikiwemo leseni ya taaluma/kazi kutoka mamlaka husika
 3. Awe na uzoefu usiopungua miaka miwili.

 MAOMBI YOTE YAAMBATANISHWE NA,

 1. Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
 2. Nakala ya cheti cha kidato cha nne au/ na cha sita au stashahada kulingana na kada ya mwombaji. Kwa aliyesoma nje ya nchi au mitaala ya nje ya nchi waambatanishe cheti cha ithibati kutoka baraza la mitihani Tanzania (NECTA).
 • Nakala ya vyeti vya Taaluma na Transcript, Aidha waliosoma vyuo vya nje ya nchi, waambatishe cheti cha Ithibati kutoka TCU.
 1. Wasifu (CV).
 2. Picha ndogo (passport size) moja ya hivi karibuni.
 3. Nakala ya kitambulisho cha uraia (NIDA/ Namba ya NIDA).
 • Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako Pamoja na cheti cha kuzaliwa na NIDA hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa viapo na kusajiliwa na Msajili wa hati, wizara ya Ardhi na maendeleo ya makazi.

NAMNA YA KUTUMA MAOMBI.

Maombi yote yatumwe ndani ya wiki mbili tangu tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili (mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 16/02/2023). Maombi yote yatumwe kwa ofisi ya Katibu Mkuu-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki S.L.P 10 LUSHOTO Au kwa barua Pepe : This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.