Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu amewasihi wazazi na walezi wenye watoto waliofaulu kwenda kidato cha kwanza kuhakikisha watoto wanakwenda shule ili kupata haki yao ya kupata elimu.

Ameyasema hayo katika Ibada ya Jumapili ya tarehe 29/01/2023 iliyofanyika katika Jimbo la Kusini Usharika wa Mamba na kuwakumbusha waumini kuwa ni jukumu na wajibu wa kila mzazi au mlezi kumpatia mtoto wake elimu.

Hata hivyo Askofu Dkt. Mbilu amewataka pia waumini wote wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na jamii kwa ujumla kuhakikisha kila mmoja anajiunga na bima ya Afya kwa wote pindi Serikali itakapo kamilisha mchakato huo wenye lengo la kutaka kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na bima.