Print

Ufunuo 14:13 “Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.

Picha za matukio mbalimbali ya Ibada ya Mazishi ya Mwalimu Wahaki Tawi Vesso, iliyofanyika leo tarehe 27/05/2023 katika Jimbo la Pwani Usharika wa Kana, Ibada hii iliongozwa na Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, mwili wa Mwalimu Wahaki Tawi Vesso umezikwa katika makaburi yaliyopo Gofu-Goseji-Tanga,

Marehemu Mwalimu Wahaki Tawi Vesso, alizaliwa tarehe 01/05/1942 na kuitwa mbinguni siku ya  Alhamisi 24/05/2023 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo  akiwa anapatiwa matibabu.

Katika kipindi cha uhai wake aliwahi kuitumikia KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki katika nafasi mbalimbali ikiwemo, Mjumbe wa Halmashauri Kuu KKKT-DKMS, Mjumbe wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Bangala, Katibu wa kamati ya Uhusiano ya Usharika kati ya Usharika wa Kana na Berlin Staken Ujerumani pamoja na mwimbaji wa kwaya Kuu ya Usharika wa Kana.

Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki unaendelea kutoa pole kwa,familia ya marehemu   ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo. BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.

Hits: 3618