Tarehe 27/08/2023 imekuwa siku ya baraka tele kwa washarika wa Jimbo la Kusini ,Usharika wa Irente kwani vijana wapatao 36 wamebarikiwa huku mmoja kati yao akibatizwa. Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu ndiye aliyeongoza Ibada hiyo. Katika Risala ya vijana hao waliobarikiwa kwa Baba Askofu Dkt. Mbilu , wamekiri kufundishwa Biblia kwa ujumla wake , mtaala wa kitabu cha pokea chapa ya Kristo na vitabu vingine, katekisimo ndogo ya Martin Luther , nyimbo za Ibada na Liturgia katika kitabu cha Tumwabudu Mungu Wetu na kuahidi kuwa imani yao sasa ni thabiti na kamwe hawata tikiswa na ulimwengu na wataendelea kuwa wafuasi na wanafunzi chini ya mwalimu mkuu yaani Yesu Kristo hadi hapo atakaporudi kulichukuwa kanisa lake.