
Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 13 wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri (LWF) Duniani, ambao ni chombo cha juu cha maamuzi unao ongozwa na kauli mbiu isemayo MWILI MMOJA, ROHO MMOJA, TUMAINI MOJA “Waefeso 4:4-6”. unafunguliwa katika Mji wa Krakow Poland leo tarehe 13/09/2023.
Mkutano huu utakuwa na jukumu la kumchagua Rais mpya wa Fungamano na Wajumbe wa Kamati mbalimbali. Rais anayemaliza muda wake ni Askofu Dkt. Panti Filibus Musa wa Kanisa la Kilutheri Nigeria.
Kutoka Bara la Afrika, Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki ni Mjumbe wa Kamati ya Ibada na Muziki iliyoteuliwa kuandaa Mkutano huu na atashiriki kuongoza nyimbo za utamaduni wa Kiafrika.Kamati hii iliundwa mwaka 2021 na ofisi ya Katibu Mkuu wa Fungamano la Makanisa ya Kilutheri Duniani ambayo makao Makuu yake yapo Geneva Uswis. Kamati hii ina wajumbe kumi kutoka Ujerumani,Canada,Norway,Hungary,Poland,Hong Kong,USA,Brazil,Switzeland na Africa ambapo mjumbe muwakilishi ni Askofu Dkt. Msafiri Mbilu.
Hata hivyo, Mkuu wa KKKT Baba Askofu Dkt. Fredrick Onael Shoo anawakilisha Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania akiambatana na Katibu Mkuu KKKT Mhandisi Robert Kitundu na wajumbe wengine 10 kutoka makundi mbalimbali kama vile Vijana na Wanawake.
