KANISA LA KINJIILI LA KILUTHERI TANZANIA
DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI
S.L.P 10, LUSHOTO.
NAFASI YA KAZI
Tarehe 19 Juni 1963, Kanisa la Usambara - Digo na makanisa mengine sita ya Kilutheri yaliungana na kuunda Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Leo hii KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (KKKT-DKMs) ni miongoni mwa Dayosisi 27 ndani ya KKKT. Dayosisi inaitwa hivyo kwakuwa inapatikana Kaskazini Mashariki mwa Tanzania katika Mkoa wa Tanga. Kwahiyo KKKT-DKMs ni taasisi ya kidini iliyosajiliwa tarehe 19 Juni 1963 na Makao yake Makuu yapo Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga. Dhamira ya KKKT-DKMs ni kufundisha na kuhubiri neno la Mungu na kutoa huduma nzuri kiroho, kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii kwa watu. Taasisi hii inatoa tangazo la kazi kwa nafasi ifuatayo:
MTOA TIBA KWA VITENDO (OCCUPATIONAL THERAPIST) (1)
MAJUKUMU YA MUOMBAJI
- Kumchunguza mgonjwa ili kutumbua na kupanga tiba kwa vitendo.
- Kutekeleza tiba kwa vitendo kwa mgonjwa.
- Kukusanya na kutunza takwimu na taarifa za mgonjwa.
- Kutunza vifaa vya idara
- Kutoa elimu ya afya kwa jamii kuhusu kutambua dalili na kuzuia ulemavu.
SIFA ZA MWOMBAJI
- Elimu ya stashahada ya Mtoa Tiba kwa vitendo kutoka chou kinachotambuliwa na serikali.
- Lazima awe na leseni toka chama chake cha kitaaluma.
- Ajue kutumia computer
- Mwenye moyo wa kufanya kazi kwenye mazingira yoyote.
- Umri kuanzia miaka 25 na isiyozidi 40
NAMNA YA KUTUMA MAOMBI. Barua ya maombi iambatanishwe na nakala za vyeti vya Elimu, wasifu wa mwombaji (Cv), cheti cha kuzaliwa, na nakala za vyeti vyote vya ujuzi mbalimbali (kama unavyo).
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 24/11/2023
- Waombaji watakaokidhi vigezo ndio watakaoitwa kwenye usaili (Interview)
Tarehe ya usaili watajulishwa kwa njia ya
Maombi yote yatumwe kwa Katibu Mkuu-KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki S.L.P 10 LUSHOTO Au: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.