MATUKIO KATIKA PICHA:-Washa ya viongozi wa Makanisa wanachama wa UEM kwa ukanda wa Afrika nzima. Washa hii inayofanyika Katika Ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Protea Jijini Dar es Salaam, mkazo wake nikuona jinsi ya kuweka mipango thabiti mara baada ya kustaafu kwa watumishi wa Kanisa. Katika semina hiyo masomo mengi yamefundishwa yakionyesha mifano mbalimbali ya jinsi watumishi wa Kanisa wanavyotunzwa wanapostaafu huko Ulaya (Ujerumani), Asia na Afrika. Pamoja na mambo mbalimbali yaliyo fundishwa na kujadiliwa katika semina hiyo, pia washiriki wamejengewa uwezo na ufahamu wa pamoja kwa kuona ni kwa jinsi gani Makanisa yanaweza kushirikiana kujengeana uwezo mapema wa namna ya kuwatunza Wastaafu.