Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewataka Wazee wa Kanisa kutambua nafasi na wajibuwao walio nao katika kulitumikia Kanisa huku akiwasihi Washarika kutoa ushirikiano kwa wazee hao ikiwa ni pamoja na kuwatia moyo ili waweze kutimiza majukumu na wajibu walioitiwa.
Askofu Dkt. Mbilu ameyasema hayo mara baada ya Ibada ya Jumapili iliyofanyika Kanisa Kuu Lushoto iliyoambatana na tendo la kuwaingiza kazini wazee wa Kanisa wa Usharika wa Kanisa Kuu Lushoto wapatao 63 huku akiwakumbusha kuwa wajibu waliopewa niwajibu wa heshima katika kuwaongoza watu wa Mungu.
Kwanyakati tofauti baadhi ya wazee wakanisa waliyoingizwa kazini katika Usharika huo wamesema kuwa wanamshukuru Mungu kwa nafasi na wajibu waliopewa katika Kanisa huku wakiahidi kushirikiana na Washarika katika kuitenda kazi ya Mungu
Katika hatua nyingine Askofu Dkt. Mbilu ametoa wito kwa Wakristo kutoa ushirikiano na kumuunga mkono Mkuu Mpya wa KKKT aliyeingizwa kazini hivi karibuni ,Baba Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, ili aweze kutimiza malengo na maono mbalimbali aliyokuwa nayo.