Print

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, yupo ziarani nchini Ujerumani, ambapo akiwa nchini humo atashiriki Ibada ya kumuaga Katibu Mkuu wa chama Cha kiinjili Cha kimisioni (UEM) anayemaliza muda wake Mch.Volker Dally na kuingizwa kazini kwa Katibu Mkuu mpya wa UEM Mch. Dkt. Andar Parlindungan,ambaye awali  alikuwa Katibu mtendaji wa idaraya mafunzona uwezeshajiwa UEM.Ibada itafanyika tarehe 01/03/2024 

Mara baada ya Ibada hiyo ya kuingizwa Kazini kwa Katibu Mkuu wa UEM, Askofu Dkt. Mbilu atatembelea na kufanya mazungumzo ya juu ya maendeleo na kukuza ushirikiano na marafiki wa Dayosisi yetu akianzia Ofisi Kuu ya Kanisa la Westephalia, Kituo cha Bethel, Jimbo la Vlotho na baadaye Jimbo la Minden.

 UEM: United Evangelical Mission ni chama Cha kiinjili Cha kimisioni ambacho kilianzishwa mwaka 1996 na wamisionari kutoka Ujerumani wa Rhenish na Betheli ambao walifika Africa, na Asia kwa ajili ya kuanzisha shughuli za Dini. Katika Africa walifika katika nchi 7 ambazo ni Tanzania, DR Congo, Africa ya Kusini, Botswana, Cameroon, Namibia na Rwanda kukiwa na madhehebu 15. Katika Tanzania inawakilishwa na Makanisa 4 ya KKKT ambayo ni KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani pamoja na KKKT Dayosisi ya Karagwe.

Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu (wa pili kutoka Kushoto), Mch. Dkt.  Andar Parlindungan (wa kwanza kutoka Kushoto),Mwenzi wa Askofu Mbilu Mwl. Mary Mbilu (wa tatu kutoka Kushoto) pamoja na Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mgharibi ambaye pia ni  Moderator wa UEM, Mch Dkt.Abednego Keshomshahara (wa nne kutoka Kushoto)

Hits: 9119