Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 16/03/2024, ameongoza Ibada ya ufunguzi wa Usharika mpya Mteule wa Saunyi uliopo katika Jimbo la Magharibi, Ibada iliyoambatana na tendo la kuwabariki vijana wa Kipaimara 201 pamoja na kufungua nyumba ya Mtumishi.
Kwa takribani miaka 38, Usharika Mteule wa Saunyi ulikua chini ya Usharika wa Gombero kati ya maeneo ya Misioni yaliyopendekezwa na Halmashauri Kuu ya Dayosisi mwaka 1986. Na mwaka 2022 Halmashauri Kuu ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ilipokea pendekezo na kulikubali la Saunyi kuwa Usharika Mteule unao hudumiwa na Mchungaji Mstaafu Denis Hiza.
Sambamba na hilo,Askofu Dkt. Mbilu amesisitiza Washarika wa Usharika Mteule wa Saunyi na Wakristo kuendelea kuliishi neno la Mungu na kujifunza kwa usahihi wake ili kuepukana na mafundisho potofu hasa hasa kuepukana na manabii wa uongo wanao hubiri mafundisho kuhusu Nuru ya Wamasai, amesisitiza kwamba,Mungu habagui kwa kabila na hakuna Mungu wa eneo moja bali Mungu ni wa wote.
Mmoja wa Washarika waliohudhuria Ibada hiyo pamoja na changamoto za barabara ambapo iliwalazimu kukaa njiani kwa takribani masaa tisa,walimshukuru Askofu Dkt Mbilu kwa moyo wa kujituma na kumtumikia Mungu kwa kusema kuwa"mbali na kuwa na ratiba ngumu ya safari ya nje ya Nchi lakini bila kupumzika amewathamini na kuwajali kwa kufika katika Ibada,Mungu aendelee kumuinua na kumbariki zaidi na zaidi.Alisema msharika huyo.
Pamoja na kuahidi kulishika neno la Mungu walilofundishwa kwa usahaihi wake wameahidi kutoyumbishwa na mafundisho potofu yalio tanda katika ulimwengu huku wakichangia deni la Dayosisi kiasi cha Tsh. 150,000 na baadae kuungwa mkono na wazazi na walezi na kufanya jumla kuu kuwa Tsh.540,000.