Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, leo tarehe 30/06/2024 ameongoza Ibada ya Kustaaafu kwa heshima kwa Mch. Lewis Fredrick Shemkala hii ikiwa ni kwa mujibu wa Katiba ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mchungaji Lewis Fredrick Shemkala, amefikia umri wa kustaafu baada ya kuitumikia Dayosisi hii kwa miaka 33 ya Uchungaji na miaka 2 ya Uinjilisti.
Akizungumza katika Ibada ya Kustaafu ya Mchungaji Lewis Shemkala iliyofanyika katika Usharika wa Makorora-Tanga kwa niaba ya wana KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, amempongeza na kumshukuru Mch. Shemkala kwa kuwa aliitikia na kukubali kutumika miaka 33.Katika utumishi wake kama Mchungaji na Miaka 2 ya Uinjilisti.
Askofu Dkt. Mbilu aliongeza kwa kusema kuwa, Wakati wa utumishi wa Mchungaji Mstaafu Shemkala alijionesha kuwa mtumishi mwenye maono, uhodari na msimamo usioyumba wa kutetea Injili na Umoja wa Dayosisina pia alitoa mchango mzuri si kwenye Kanisa tu, bali pia kwenye jamii katika maeneo yote ambayo Mungu alimpa neema ya kutumika.
Sambamba na hayo amemkumbusha Mchungaji Mstaafu kwamba bado katika Dayosisi, Jimbo na Usharika utakaomtunza kiroho, ana uhakika kwamba ataendelea kuwa mtumishi mwema wa Kristo, kutashauri na kuelekeza, hata kupanga na kutekeleza yahusuyo imani, uchumi, na huduma za huruma na za maendeleo kwa jamii.
Askofu Dkt. aliongeza kwa kusema kuwa Wakati utumishi wa Mchungaji Mstaafu Shemkala alijionesha kuwa mtumishi mwenye maono, uhodari na msimamo usioyumba wa kutetea Injili na Umoja wa Dayosisina pia alitoa mchango mzuri si kwenye Kanisa tu, bali pia kwenye jamii katika maeneo yote ambayo Mungu alimpa neema ya kutumika.
Kwa upande wake Mch. Msaafu Lewis Shemkala, wakati wa itikio lake amesema kuwa anamshukuru Mungu aliyemuwezesha kutumika katika nafasi ya Uchungaji na kupewa heshima ya kustaafu kwa heshima baada ya kutimiza umri wa kustaafu wa miaka sitini na baada ya kutumika shambani mwa BWANA kwa miaka 33 ya Uchungaji na Miaka 2 ya Uinjilisti.
“Kipekee na kwa Moyo wa Dhati napenda kumshukuru Mke wangu Mwinjilisti NEEMA BENDERA,pamoja na Watoto wangu kwa kunitia moyo na kuniombea katika kipindi hiki chote cha utumishi huu nilioitiwa .
Pia napenda kuushukuru Uongozi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, chini yako Baba Askofu Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, kwa kutenga muda na kuandaa utaratibu wa Ibada hii.
Napenda pia kuwashukuru Wachungaji wenzangu, Mashemasi, na Wathelojia ambao tumetumika kwa pamoja shambani mwa Bwana.
Nawashukuru Parishwokers, Wainjilisti,Wahasibu, Walimu wa Mitaa, wazee wa Kanisa, walimu wa Shule ya Jumapili, wajumbe wa kamati mbalimbali za sharika tuliotumika pamoja katika kipindi chote cha Utumishi shambani mwa Bwana.
Kwa dhati ya moyo wangu ninapenda kuwashukuru Wazazi wangu, ndugu zangu wote ,Washarika wa sharika nilizotumika na Wakristo wote,marafiki na jamaa wote kwa kunitia moyo katika kuitenda kazi ya Mungu na kipekee sana Usharika wa Makorora ambao unaandika Historia katika maisha yangu ya kuwa Usharika niliostaafu.
Ninawashukuru sana Kamati ya maandalizi chini ya uongozi wa Dkt. Brunno Mmbando; kwa kuratibu shughuli hii. Ninawashukuru sana endeleeni kuifanya kazi ya Mungu kwa Umoja Furaha na Amani na BWANA mwenyewe atawabariki.
Mbali na kupewa heshima hii ya kuwa Mchungaji Mstaafu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, baada ya kutumika kwa kipindi cha miaka 33 ya Uchungaji na Miaka 2 ya Uinjilisti. Naahidi kuwa nitaendelea kushirikiana na Uongozi wa Dayosisi, watumishi wenzangu pamoja na washarika wote katika kumuabudu Mungu na Kumshuhudia Kristo siku zote za Maisha yetu.
Katika kipindi hiki cha utumishi nimepata ushirikiano mzuri wa viongozi wa Serikali, kukaribishwa katika matukio mbalimbali yakiwemo ya Viongozi wa Kitaifa. Hivyo ninapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa ujumla wao kwa namna tulivyoshirikiana.
Sambamba na Shukrani hizi niombe tuendelee kumuombea Kiongozi wetu wa Nchi, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bunge na Mahakama ili Mungu mwenyewe aendelee kuwapa hekima viongozi hawa wa mihimili hii ya nchi yetu ili Amani, Utulivu na haki vitawale na watanzania wote wafaidi Maendeleo ya nchi hii.” Mwisho niwashukuru ninyi nyote mliohudhuria Ibada hii ya kustaafu kwangu Mungu awabariki sana. Asanteni sana karibuni nyumbani Handeni” Alisema Mchungaji Mstaafu Lewis Shemkala.
Mchungaji Lewis Fedrick Shemkala amekuwa mtumishi wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki tangu mwaka 1988 na alipewa wajibu mbalimbali kama ifuatavyo:- 1988 -1989 Alikuwa Mwinjilisti katika Usharika wa Korogwe na mwaka 1990 alikuwa Shemasi katika Usharika wa Kwalukonge.
Tarehe 30 June, 1991 alibarikiwa kuwa mchungaji katika Ibada iliyoongozwa na Hayati Baba Askofu Dkt. Sebastian Kolowa, Ibada iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Shule ya Sekondari Lwandai-Mlalo, Lushoto. Siku ambayo pia Dayosisi ilikuwa inaadhimisha miaka mia moja ya Injili.
Mchungaji Lewis Fedrick Shemkala alibarikiwa kuwa Mchungaji tarehe 30/06/1991 katika Ibada iliyo ongozwa na Hayati Baba Askofu Sebastiani Kolowa, Ibada iliyofanyika katika uwanja wa Michizo wa Shule ya Seondari Lwandai Mlalo Lushoto siku ambayo pia Dayosisi ilikuwa inaadhimisha miaka mia moja ya Injili. Mchungaji Shemkala ametumika katika Sharika mbalimbali kama ifuatavyo.
02/07/1991 - 11/01/1993 Usharika wa Mamba Soni
12/01/1993 - 31/12/1995 Usharika wa Mlalo
1996 - 1999 Chuo cha Theologia Motheco-Mbeya
12/01/2000 - 30/04/2006 Usharika wa Mtae
01/05/2006 - 15/06/2012 Usharika wa Kana na Mkuu wa Jimbo la Pwani na kitengo cha mabaharia kwa miaka 2
16/06/2012 - 25/06/2021 Usharika wa Handeni
26/01/2021 - 30/04/2022 Usharika wa Hale01/05/2022-30/06/2024 Usharika wa Makorora.