Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewakumbusha Wachungaji pamoja na Mashemasi juu ya wito walioitiwa katika kumtumikia Mungu kwa uaminifu wote.
Askofu Dkt. Mbilu ametoa wito huo tarehe 04/07/2024 akiwa anafungua mkutano wa Wachungaji na Mashemasi unaofanyika katika Jimbo la Magharibi Usharika wa Mkata ulioandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki na kusema kua kila Mtumishi ano wajibu wa kutumika sawa sawa na wito ambo Mungu amemuitia.
Katika hatua nyingine Askofu Dkt. Mbilu amewataka Wachungaji pamoja na Mashemasi kuendelea kuombea uchanguzi wa Serikali za Mitaa na uchaguzi Mkuu utakao fanyika mwaka 2025 huku akiwasihi waumini kujitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali katika chaguzi hizo pamoja na kujitokeza katika kupiga kura wakati wa uchaguzi utakapofika.
Aidha Baba Askofu Dkt. Mbilu amesema ili uwe na sifa ya kupiga kura ni lazima ujiandikishe katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,Awe ana kadi ya mpiga kura iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, pamoja na hayo akatoa wito kwa kila msharika mwenye sifa ya kupiga kura kuhakikisha anajitokeza katika zoezi uboreshaji wa daftari la mpiga kura ili kujiandaa kwaajili ya kushiriki katika kupiga kura.
Mkutano huo wa Wachungaji na Mashemasi umeanza rasmi leo na utahitimishwa siku ya Jumapili ya tarehe 7/7/2024 kwa ibada maalumu ya kuwabariki Wathiologia watano wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ambao watabarikiwa kuwa wachungaji, ibada hiyo itaongizwa na Askofu Dkt Msafiri Joseph Mbilu.