HABARI KWA UFUPI.

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwajali na kuwahudumia Wananchi katika sekta ya Afya kwa kujenga Hospital kubwa ya Wilaya ya Handeni iliyopo katika Kijiji cha Mkata, kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo kutoka ndani na nje ya Nchi.

Askofu Dkt. Mbilu ametoa pongezi hizo tarehe 06/07/2024 alipotembelea Hospital hiyo na kujionea miundombinu ya kisasa ambayo imekua msaada mkubwa kwa Wananchi mbalimbali katika Wilaya hiyo.

Amesema uwepo wa Hospital ya Bumbuli, Hospital ya wagonjwa wa Afya ya akili ya Lutindi (Lutindi Mental Hospital), Zahanati pamoja na shule mbalimbali ambazo zinamilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, ni kuonyesha kuwa Dayosisi iko bega kwa bega na Serikali katika kuwahudumia Wananchi.

Aidha Askofu Dkt. Mbilu amewasisitiza wafanyakazi katika Hospital hiyo wakiwemo Madaktari kuhakikisha wanatumia na kutunza vyema miundombinu pamoja na vifaa mbalimbali vilivyopo katika Hospital hiyo ili viendelee kuboresha huduma za kisasa kwa kuwahudumia Wananchi.



