

Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, amewataka Wachungaji waliobarikiwa pamoja na Watumishi wengine wa Kanisa kuendelea kukemea matendo maovu na mafundisho potofu ya neno la Mungu yaliyotanda katika jamii na ulimwengu kwa ujumla ili kuwezesha jamii kuendelea kuishi kwa amani na utulivu.

Wito huo umetolewa na Askofu Dkt. Msafiri Mbilu,kwenye Ibada ya Jumapili ya tarehe 07/07/2024 iliyoambatana na tendo la kuwabariki na kuwaingiza kazini wachungaji wapya watano, Ibada iliyofanyika katika Jimbo la Magharibi Usharika wa Mkata na kusema kuwa Wachungaji wanaitwa kwenda kutumika hivyo wana wajibu wa kuhakikisha wanasimamia na kufundisha mafundisho sahihi ya neno la Mungu na kukemea maovu katika jamii.

Aidha amewataka kuwa tayari wakati wote kwenda mahali popote wanapotumwa ili kuitenda kazi ya Bwana sambamba na kuwasihii washarika kutokuwachanganya Wachungaji walioitwa katika wito wa kumtumikia Mungu mahali popote na badala yake wanapaswa kuendelea kuwaombea ili waweze kuifanya kazi ya Mungu sawa sawa na wito walioitiwa.

Halikadhalika amesema Wachungaji wameteuliwa kuwa viongozi hivyo wana wajibu wa kusimamia maendeleo katika jamii na kukemea wote wanao jiingiza katika vitendo viovu ikiwemo ujambazi, matumizi ya madawa ya kulevya na ukatili katika jamii.

Katika Ibada hiyo ambayo sehemu ya Mahubiri iliongozwa na Mch Dkt. Albrecht Philips wa Kanisa la Westphalia (Evangelical Church of Westphalia) Ujerumani, unaoongozwa na . umla ya Watheologia watano wamebarikiwa na kuingizwa kazini na kuwa Wachungaji ambao ni MCH. EVELINE MWAMBASHI KUYONGA, MCH, DAVID MARTIN MMBALI, MCH.JUSTINE ERNEST MHOMBO, MCH. NICOLAUS HENDRISH ABIHUDI PAMOJA NA MCH. RIZIKI JOHN KIGARAMA.

