HABARI PICHA:
Askofu wa KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Mch Dkt. Msafiri Joseph Mbilu, akiwa ameongozana na ugeni kutoka Kanisa la Westphalia (Evangelical Church of Westphalia) Ujerumani, unaoongozwa na Mch Dkt. Albrecht Philips.
Ugeni huo ambao unafanya ziara ya kuitembelea KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,kwa siku mbili na tarehe 07/07/2024 wamepata nafasi ya kutembelea Hospital ya Bumbuli inayomilikiwa na KKKT-Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, na kujionea miundombinu na huduma inayotolewa Hospitalini hapo.
Baada ya kujionea huduma zinazotolewa Hospitalini hapo Mch Dkt. Albrecht Philips kwa niaba ya ujumbe alioambata nao ameahidi kuendelea kushirikiana na Uongozi wa Dayosisi katika kuboresha huduma Hospitalini hapo ikiwa ni pamoja na kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa kupitia marafiki mbalimbali.